PROPOSAL
UANZISHWAJI WA CCM KWANZA BLOG & ONLINETV
(SAUTI YA JAMII)
Naomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iniruhusu kuanzisha CCM KWANZA Blog & OnlineTV kwa lengo la kupanua wigo wa mitandao ya chama ili iwafikie wananchi wengi wa rika mbalimbali kwa kuanzia msimu unaokuja wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025.
Blog itakuwa na mambo mengi muhimu ya chama na serikali pamoja na kijamii ambapo pia itapambwa na picha za viongozi wakuu wa chama waliopo madarakani na wastaafu.
Itakuwa na Katiba ya chama, Ilani Utekelezaji ya chama na miongozo pamoja na nukuu muhimu za viongozi waliopo madarakani na wastaafu pamoja na waliotangulia mbele ya haki kwa lengo la kuihamisisha jamii na hasa vijana kujitukikia vyema cha , serikali na Taifa kwa ujumla.
Itakuwa na vionjo mbalimbali vya kuwavutia wateja kama vile nyimbo mbalimbali za hamasa za CCM, michezo na burudani vyenye maadili mema.
Tutaposti hotuba muhimu za viongozi mbalimbali na matukio mengine tutakuwa tunakwenda LIVE kwa lengo la kuzidi kuongeza viewers.
Itakuwa na sehemu ya wananchi kujiunga kidijitali uanachama wa CCM na jumuiya zake.
Tutaposti habari za kimataifa zinazoendana na maadili ya chama na sheria za nchi.
Itaunganishwa na mitandao ya kijamii; Facebook, Twitter x, Instagram, WhatsApp na mingineyo.
Tutaunda pia CCM Kwanza APP.
Tutapanua wigo zaidi kwa kupata habari zaidi kupitia kwa viongozi wa CCM na jumuiya wa mikoa, wilaya, Kata watakaokuwa wanatupatia habari za matukio mbalimbali ya chama viongozi wanapokwenda kukagua Utekelezaji wa Ilani katika miradi mbalimbali ya maendeleo.
Links za matukio hayo zitakuwa zinasambazwa pia kwenye magrupu mbalimbali ya Whatsapp na kupitia emails nilizonazo zitakazovifikia vyombo mbalimbali vya habari nchini na kuwa na uamuzi wa kuzitumia habari zetu.
MAHITAJI
1.Ili kutekeleza majukumu hayo kwa urahisi na ufanisi naomba niwe na vijana waandishi wa habari wawili wa kiume na wa kike kwa ajili ya Kuapload matukio mbalimbali na kwenda kufanya coverage ya shughuli za chama, serikali na ya kijamii.
Posho yao ianzie sh. 500,000 kwa kila mmoja.
2. Gharama za usajili wa Blog ni. sh. 500, 000 kwa ajili ya ada na sh. 50, 000 ya maombi.
3. Kuitengeneza Blog na App sh. 600,000.
4. GB 100 kila mwezi
5. Tupatiwe Ofisi, Laptop, Kamera, Stand, Microphone
6. Posho ya usafiri kwa mwezi
Nashauri kwa siku za usoni Blog ikiwa vizuri, kuwepo na kijana wa kutafuta matangazo kwa wadau, ambapo fedha zikipatikana zitasaidia kuboresha uendeshaji wa blog.
Pia nashauri yawepo makubaliano maalumu kati ya chama na mimi nitakayekuwa Msimamizi na mhariri mkuu wa Blog.
No comments:
Post a Comment