Sunday, December 17, 2023

MIPANGO YANGU YA MAENDELEO 2023-2025

 

                               MIPANGO 2023-2026

NJELELA

Mimi Richard Gissy Mwaikenda naazimia kupanga mipango yangu ya maendeleo  kuanzia mwaka huu 2023 hadi 2025 na kuendelea.

Njelela, wilayani Ludewa Mkoa wa Njombe tayari nina shamba lenye heka 10 ambalo hivi karibuni tumelipima.

Heka 3 tayari zina miche 204 na iliyoharibika miche 83 (tayari). mwezi Januari nitafidia miche hiyo 83 na kuongeza heka moja ya 4 na kupanda miche 100.Tayari.

Natarajia kuanzisha kitalu chenye miche 2000 kwa ajili ya kupanda shambani na kuuza.

Mipango yangu katika miaka miwili ijayo nipande miche mingine 500 ili ifikie 800.


2. UMWAGILIAJI

Kwa vile shamba tayari lina maji kwa ajili ya umwagiliaji, nimepanga kupanda mazao mbalimbali kwa ajili ya chakula na kuuza kwa ajili ya malipo ya wahudumiaji shamba na vilevile kupunguza gharama ya mimi kwenda kukagua shamba.

Wahudumu waliopo shamba ni Msimamizi Mkuu Mzee Gregory Mwapinga na kijana Nehemia ambaye kwa hivi sasa analipwa sh. 100,000 kwa  mwezi.

3. MAZAO

Mazao ninayotarajia kupanda ni, maharage (Tayari), mahindi, migomba ya asili 50 na ya kisasa 50.

Viazi (tayari), mihogo, Tangawizi, vitunguu na mengineyo.

Kupanda Macadamia yaani karanga pori miche  20, lengo ni miche 100.


4. UFUGAJI

Ufugaji wa nyuki kwa ajili ya kupata asali ya kuuza, natarajia kuanza na mizinga 20 ya asili na 50 ya kisasa hadi machi iwe imekamilika. Itabidi kijengwe kibanda kwa ajili ya mizinga ya kisasa.

Ufugaji wa nguruwe kwa ajili ya kupata mbolea na kuwauza kwa ajili ya kujiongezea kipato. Tutaanza na nguruwe wa kike wawili na dume mmoja, lengo ni kuwa na nguruwe zaidi ya 100.

Pia tutafuga mbuzi, kuku wa kienyeji na chotara, bata. Ujenzi wa mabanda.


             BIASHARA YA  ASALI, MAHARAGE

Natarajia kuanza biashara ya kununua asali madumu 10 hadi 20 na kuuza, pia natarajia kuanza kununua maharage na kuyauza kwenye genge letu Dar.

SPRINKLER

Kununua Sprinkler mbili za nguvu pamoja na mipira  inch 2 (tayari)

 

Mipango mingine ni kununua heka zaidi za shamba Njelela.

Kufuatilia shamba la heka 10 kwa Shikamoo Parachichi


 MUNGU NISAIDIE NIFANIKIWE


                                MIPANGO HOME DAR

1.  GENGE

Tayari banda limekamilika kinachotakiwa sasa ni mtaji ili mwanzoni mwa mwezi Januari lianze.Friji kwa ajili ya soda, maji na juisi na mizani vipo. Genge hilo litakaloendeshwa na Mke wangu kipenzi Mary litakuwa na vyakula vya aina mbalimbali yakiwemo matunda. Pia nina mipango genge hilo pauzwe mchele, maharage na viazi vitamu na mviringo kutoka mikoani.

 

2.       KUKU

Ufugaji wa kuku chotara 200 mtaji uwe sh 600,000

 

 3.UJENZI

Kuanza ujenzi wa vyumba 11 nyuma na mbele ya nyumba kwa ajili ya kupangisha. Ujenzi unatarajiwa kuanza  2026.

 

Kulipia kibao cha Mtaa Mwaikenda 135,000

Kukamilisha choo cha ndani

Kupaka rangi bati

Kujenga Kalo.

Kupiga ripu nje na kumalizia ndani tiles na slingbodi

 

MUNGU NISAIDIE

 

DODOMA

 

-Kuweka mizinga ya nyuki 10 hadi 50 katika Kijiji cha Mbwasa Manyoni.

- Kupanda mikorosho 30

- Kuanzisha PUB, kuuza nyama ya nguruwe na ufugaji pamoja na Bucha.

-Ukusanyaji mapeke

-Kununua kiwanja au shamba

 

BUNGENI

-Kuanza Uratibu wa ziara za shule  Bunge 2026

-Kuongeza idadi ya marafiki wabunge wapya, mawaziri kuongeza kipato

-Kuanzisha utaratibu wa kuwatengenezea albamu

 

MENGINEYO

=Kuongeza urafiki na wakuu wa wilaya

-Kuongeza idadi ya taasisi za kufanya nazo kazi kuanzia 10 hadi 20

-Kuiboresha Kamanda wa Matukio na kuanzisha ya michezo SUPASPOTI TV

-Kusajili Jukwaa Huru la Wahariri Tanzania (JUWATA). Tayari.

 

RUFIJI

-Kugomboa shamba Heka 10 katika Kijiji cha Chumbi

Kupanda mikorosho 300

 

BAGAMOYO

Kusafisha shamba heka 3 katika Kijiji cha Masugulu

 

MUNGU NISAIDIE

 

No comments:

Post a Comment