Sunday, October 16, 2022

WAFANYAKAZI WA BENKI YA NMB WAPEPERUSHA BENDERA YA NMB MLIMA KILIMANJARO


Wafanyakazi wa Benki ya NMB  wakiipeperusha bendera ya Benki hiyo wakiwa katika kilele cha Mlima Kilimanjaro, kama ishara ya kusherehekea Mwezi wa Huduma kwa Wateja.

Wafanyakazi wa Benki ya NMB pamoja na wasindikizaji wa wenzao waliopanda Mlima Kilimanjaro, wakiwashangilia wenzao waliopanda na kushuka Mlima huo kwa siku Saba, katika hafla ya mapokezi  iliyofanyika katika lango la Mweka.

Kaimu Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro – Bw. Iman Kikoti katika picha ya pamoja na timu ya Wafanyakazi wa NMB waliopanda Mlima Kilimanjaro, baada ya kuwatunuku vyeti kuashiria walifika katika  kilele cha Mlima huo mrefu Afrika – Uhuru Peak

Wafanyakazi wa Benki ya NMB wakiipeperusha bendera ya Benki hiyo yenye ujumbe ‘Huduma kwetu Shangwe’ wakiwa katika kilele cha Mlima Kilimanjaro, kama ishara ya kusherehekea huduma  wanazozitoa kwa wateja wao na jamii kwa ujumla.


……………………………

Wafanyakazi 6 wa Benki ya NMB wamefanikiwa kupanda na kupeperusha bendera ya NMB katika kilele cha Mlima Kilimanjaro kama sehemu ya kuadhimisha Mwezi wa Huduma kwa Wateja, unaoadhimishwa duniani kote kila Oktoba.

 

Benki hiyo pia, imelitumia tukio hili la kihistoria kama sehemu ya kuwahamasisha wafanyakazi wake na Watazania kwa ujumla kushiriki utalii wa ndani ili kusaidia kukua kwa shughuli hiyo yenye fursa lukuki kibiashra na tija kiuchumi. 

Tukio la kusherekea Mwezi wa Huduma kwa Wateja mita 5,895 juu ya usawa wa bahari, umekua na maana kubwa kwa namna benki hiyo inavyozingatia huduma bora kwa wateja wake na kuudhihirishia umma kuwa ni kinara wa kutoa masuluhisho mbali mbali kwa wateja wake, ikiwemo kuwawezesha kuteleza kidijitali mahali popole na wakati wowote kupitia NMB Mkononi (Piga *150* 66# au App), Lipa Mkononi (QR) na NMB Direct.

Timu hiyo ya NMB imetumia siku saba kupanda na kushuka Mlima Kilimanjaro wakianzia lango la Machame na kumalizia lango la Mweka, walipokelewa na wenzao kutoka ofisi ya Kanda ya Kaskazini pamoja na matawi ya Moshi.

Aidha, hiki kimekuwa ni kitendo cha kutambua umuhimu wa biashara ya utalii na jukumu la msingi kwa sekta hiyo katika uchumi wa taifa na maendeleo ya nchi kwa ujumla.

 

Akizungumza wakati wa kuwapokea wafanyakazi hao kutoka mlimani, Kaimu Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro – Bw. Iman Kikoti alisema kuwa, kitendo cha wafanyakazi wa NMB kupanda Mlima Kilimanjaro kinaimarisha nafasi ya benki hiyo kuendelea kuwa karibu na sekta ya utalii na mshirika wa kimkakati wa maendeleo ya taifa.

 

Pia alibainisha kuwa, uamuzi wa NMB wa kuhamasisha utalii wa ndani ni kielekezo cha utayari wake kuchangia maendeleo na ustawi wa tasnia hiyo ili iweze kuchangia kikamilifu kuchochea kukua kwa uchumi nchini na ujenzi wa taifa. Bw. Kikoti aliipongeza NMB kwa hilo huku akisisitiza kuwa utalii wa ndani ni hazina kubwa kwa taifa ambayo inahitaji ushirikiano wa wadau kuufanya kushamili na kuchangia kukua kwa sekta nzima ya utalii nchini.

 

“Kwa sasa mchango wa utalii bado ni mdogo kwa hiyo uamuzi wa NMB kusaidia kuuchangamsha ni jambo jema na la kimaendeleo linalopaswa kuungwa mkono na wadau wote wa sekta binafsi,” alibainisha.

 

Nae kiongozi wa safari hiyo ambaye ni Afisa Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB, Bw. Alfred Shao, alisema kamwe hawatajutia kushiriki kwenye zoezi hilo lilowafunza mambo mengi ya kimaisha na kikazi.

Tuesday, June 14, 2022

CV YANGU

 

         

           CV-TAARIFA YANGU KWA UFUPI


Jina: RICHARD GISSY MWAIKENDA


KOZI TAALUMA YA UPIGAJI PICHA

    -World Press Photo -2002

    -Fredrick Noumann Foundation-1999

    -Wizara za Elimu na Utamaduni-1999

    -Imaging Our Invironment-SADC Region-1997

    -Goethe-Institute -1994


TUZO MBALIMBALI

  -Mpigapicha Bora Tanzania (EJAT) 2009

  -Mshindi wa Pili uandishi Makala Habari za Michezo (EJAT)-2014       

  -Mpigapicha Bora wa Pili Tanzania Michezo (EJAT)-2010


USHIRIKI MATUKIO MAKUBWA

    -Mwandishi wa Habari Mbio za Mwenge Nchi Nzima-2001

    -Kampeni za Uchaguzi Mkuu Tanzania Bara/Visiwani 1995-2015

UTEUZI

Niliteuliwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye kuwa Mjumbe wa Kamati ya Kutathmini Hali  ya Uchumi ya Vyombo vya Habari na Wanahabari- Machi 2023.


    -COVERAGE YA VIONGOZI MASHUHURI DUNIANI

-Eg.George Bush

      -Barrack Obama wa Marekani, XI Jimping wa China...


KAZI

   -Kampuni ya Business Times-Majira 1994-2009

   -Gazeti la Jambo Leo 2009-2017

   -Soka Magazine- 2002

    -Kamanda wa Matukio Blog-Mmiliki

    -Mhariri Blog ya Taifa ya CCM (CCM BLOG)-2018-Hadi sasa 


KUZALIWA 

  -Kandete, Rungwe mkoani Mbeya 1964


ELIMU

  -Msingi-Kandete, Rungwe mkoani Mbeya

          -Madenge, Temeke, Dar es Salaam

  -Sekondari-Azania, Ilala, Dar es Salaam


Nimeambatanisha na kopi za vyeti vya Taaluma

     

     

Tuesday, January 25, 2022

NIKIWA NA RAIS JOHN MAGUFULI 2015

Nikijadiliana jambo baada ya kuteuliwa kuwa mgombea urais kupitia CCM 2015. Nilipewa jukumu la kuwa Mwenyekiti wa waandishi wa habari kwenye kampeni  zake.

 

MIMI NA RAIS JAKAYA KIKWETE

2012  nyumbani kwa Rais Ikulu baada ya familia ya Kikwete  na familia yake kuandikishwa sensa ya watu.
Akipokea mchango wanu wa sh. 10,000 Ikulu Dar es Salaam kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa hosteli Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Akiniambia jambo wakati wa mahafali ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam-DUCE Changombe
 

CV-TAARIFA YANGU KWA UFUPI


 CV-TAARIFA YANGU KWA UFUPI


Jina: RICHARD GISSY MWAIKENDA


KOZI TAALUMA YA UPIGAJI PICHA

    -World Press Photo -2002

    -Fredrick Noumann Foundation-1999

    -Wizara za Elimu na Utamaduni-1999

    -Imaginga Our Inviroment-SADC Region-1997

    -Goethe-Institute -1994


TUZO MBALIMBALI

  -Mpigapicha Bora Tanzania (EJAT) 2009

  -Mshindi wa Pili uandishi Makala Habari za Michezo (EJAT)-2014       

  -Mpigapicha Bora wa Pili Tanzania Michezo (EJAT)-2010


USHIRIKI MATUKIO MAKUBWA

    -Mwandishi wa Habari Mbio za Mwenge Nchi Nzima-2001

    -Kampeni za Uchaguzi Mkuu Tanzania Bara/Visiwani 1995-2015

    -Coverage ujio wa Viongozi Mashuhuri Duniani Eg.George Bush

      Barrack Obama wa Marekani, XI Jimping wa China...


KAZI

   -Kampuni ya Business Times-Majira 1994-2009

   -Gazeti la Jambo Leo 2009-2017

   -Soka Magazine- 2002

    -Kamanda wa Matukio Blog-Mmiliki

    -Blog ya Taifa ya CCM (CCM BLOG)-2018-Hadi sasa 


KUZALIWA 

  -Kandete, Rungwe mkoani Mbeya 1964


ELIMU

  -Msingi-Kandete, Rungwe mkoani Mbeya

          -Madenge, Temeke, Dar es Salaam

  -Sekondari-Azania, Ilala, Dar es Salaam